Subscribe Us

header ads

TATIZO LA MAAMBUKIZI KWENYE VIA VYA UZAZI(P.I.D) NA SULUHISHO LAKE.

TATIZO LA MAAMBUKIZI KWENYE VIUNGO VYA UZAZI( PID) NA SULUHISHO LAKE


Maambukizi kwenye njia ya uzazi au kwa kifupi PID, ni mambukizi ya bacteria yanayoathiri sana wanawake kwenye mfumo wa uzazi. Na kuweza kuleta athari katika sehemu zozote kwenye njia ya uzazi.moja ya athari za PID  ambayo wanawake hupata ni kutoweza kushika mimba yaani ugumba. Tafiti zinasema kati ya wanawake nane walaiowahi kuugua PID basi mmoja wao atakutana na shida kupata mimba kwa siku za hapo baadae huku wale wanaofanikiwa kupata ujauzito basi hupata matatizo pia ikiwemo mimba kuharibika au kujifungua kabla ya wakati.


NINI MAANA YA PID?


Maana halisi ya PID ni hali ya kututumka au kucharuka kwa sehemu ya njia ya uzazi kwa mwanamke, sehemu hizi ni kama mirija ya uzazi au ovary ambako kunasababishwa na magonjwa yanayosambazwa kwa njia ya ngono.

Maambukizi kwenye njia ya uzazi (PID) yana tabia ya kusambaa kutoka sehemu moja kwenda nyingine na ndio maana kuna umuhimu wa kutibu tatizo hili mapema. Maambukizi haya yanaweza kusambaa kutoka kwenye uke mpaka sehemu zingine za uzazi wa mwanamke kama mirija ya uzazi, mifuko ya mayai(ovari) na kwenye shingo ya kizazi(cervix). Maambikizi haya yanaweza kusababisha makovu kwenye mirija ya uzazi na kupelekea kupata Ectopic pregnancy ambayo ni mimba iliyotungwa na kushindwa kusafiri kuelekea kwenye mfuko wa mimba(uterus) kutokana na majeraha kwenye mirija.


DALILI ZA UGONJWA WA P.I.D


Dalili za PID zinatofautiana kwa mtu mmoja hadi mwingine. Kwa baadhi ya wanawake dalili huwa mbaya na kwa wengine dalili huwa za kawaida, wakati mwingine wanawake hukaa na ugonjwa kwa muda mrefu bila kujua kutokana na kuchanganya dalili na magonjwa mengine.zifuatazo ni dalili zinazojotokeza zaidi kwa wanawake wengi.


-Maumivu ya tumbo chini ya kitovu ambayo yanaweza kuwa upande mmmoja au pande zote kulia na kushoto

-Sehemu za uke kuwa na ulaini sana

-Kupata maumivu wakati watendo la ndoa wakati mwingine kupeleekea kuvuja damu wakati na baada ya tendo la ngono na hivyo kukosa tena hamu ya tendo la ndoa

-Kuvurugika kwa hedhi

-Kutokwa na majimaji ukeni kusiko kawaida hasa yenye rangi ya njano na kijani

-Maumivu wakati wa kukojoa

-Kupata maumivu wakati wa choo

Kupata dalili za homa kama kizunguzungu,mwili kukosa nguvu, kukosa hamu ya kula na uchovu mwingi.


-Madhara Yanayosababishwa Na Maambukizi Kwenye Njia Ya Uzazi(PID)

Maambukizi kwenye njia ya uzazi husababisha athari kubwa sana kwa mwanamke,kama tulivoona pale juu PID inaweza kusababisha ugumba na mimba kujishikiza mahali pasipo sahihi(ectopic pregnancy) tofauti na mfuko wa mimba. Kadiri unavoumwa zaidi PID ndivyo hatari ya kupata ugumba inavoongezeka. Mimba kutokea nje ya mfuko wa mimba ni ishu kubwa ya kiafya na inahitaji uangalizi mkubwa wa kidactari ili kuzuia kuvuja kwa damu na hatimae kupelekea kifo kwa mama. Madhara mengine ya PID ni

-Kupata majeraha kwenye mirija ya uzazi, majeraha yanaweza kutokea nje ama ndani, tatizo hili linaweza kuwa gumu kutibika na hutokea tu pale ambapo maambukizi hayakutibiwa kwa muda mrefu zaidi.

-Kuziba na kujaa maji kwa mrija ya uzazi(hydrosalpinx kutokana na majeraha ya tishu zake

-Maumivu ya tumbo ya muda mrefu husababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa na mwanamke kutofurahisa unyumba.

-Kuongezeka kwa hatari ya kupata matatizo mengine wakati wa ujauzito na kujifungua.

-Kama tulivokwisha kusoma kwamba PID huletekezwa kwa kiasi kikubwa na magonjwa ya zinaa ambayo hayakutibiwa vizuri (sexual transmitted diseases). Kwa hivo basi ni muhimu kufahamu dalili za magonjwa ya zinaa ambayo ni common sana kwenye jamii yetu kama gonorrhea(kisonono) na chlamydia. Ugonjwa wa Chylamidia ni ugonjwa wa zinaa unaowaathiri wake kwa wanaume na husambazwa kupitia uke, njia ya haja kubwa na pia ngono ya mdomo.


Ugonjwa Wa PID Husababishwa Na Nini? Je Zipi Ni Tabia Hatarishi Zinazopelekea Uugue PID.

Kwa kiasi kikubwa wanawake waliopo chini ya umri wa miaka 35 wanaathirika zaidi na maambukizi kwenye njia za uzazi, kutokana na kwamba wanajihusisha zaidi na ngono. Tumeona hapo juu kwamba kutokutibiwa vyema kwa maradhi ya gonorrhea na chlamydia ndio chanzo kikubwa cha PID, achilia mbali sababu hii, baadhi ya bacteria wengine wanaweza pia kusababisha PID, bacteria wengine wanaweza kuambukizwa wakati wa tendo la ngono, au wakati wa kujifungua, au kwenye kitendo cha utoaji mimba na kisha wakajificha kwenye njia ya uzazi wakaanza kukua taratibu na kusambaa.baadhi ya bacteria ambao wamegundulia kusababisha PID ni hawa wafuatao

-Chlamydia trachomatis

-Neisseria gonorrheae

-Mycoplasma genitalium


VIHATARISHI VYA PID

Kundi la wanawake wenye umri kati ya miaka 25 mpaka 35

Kufanya ngono bila kinga

Wanawake waliowahi kuugua PID huko nyuma ama kupata maambukizi mengine ya bacteria kwenye njia ya uzazi.

Kusafishwa kizazi mara kwa mara na matumizi ya kemikali kujisafisha ukeni, kitendo ambacho kinaharibu bacteria wazuri na kusababisha ukuaji wa bacteria wabaya na fangus

Matumizi ya kitanzi kwa ajili ya kupanga uzazi

Kuugua UTI mara kwa mara, na wanawake waliwahi kutoa mimba wapo kwenye hatari zaidi ya kupata PID

Uvutaji wa sigara na madawa ya kulevya.


Hatua 4 Zifuatazo Zitakusaidia  Kuzuia Kupata Maambukizi Kwenye Njia Ya Uzazi (PID) Na Magonjwa Ya Zinaa


-Fanya ngono salama kwa kutumia kinga na kuishi na mpenzi mmoja mwaminifu.

hii ni hatua muhimu ya kwanza na ya uhakika zaidi katika kuzuia kupata PID maana tayari tumeshaona hapo juu kwenye makala yetu njia kubwa ya kusambaa kwa maambukizi ni ni njia ya ngono. Kama ukichagua kuwa na wapenzi wengi basi hakikisha unavaa condom kwa kila tendo. Kama una mpenzi mmoja na kati yenu kuna ambaye kaugua basi hakikisheni mnaacha kufanya ngono mpaka pale mtakapotibiwa mkapona kabisa.


-Hakikisha unafanya vipimo kwa magonjwa ya zinaa na kuyatibu haraka iwezekanavyo

wataalamu wa afya wanashauri kwamba watu walioko chini ya miaka ishirini na tano wafanye vipimo kila mwaka kwa magonjwa ya zinaa kama chlamydia. Wanawake wenye wapenzi wengi wanatakiwa kuonana na mtaalamu wa magonjwa ya wanawake(gynecologist) kwa vipimo kugundua uwepo wa vimelea vya magonjwa ya zinaa.ni muhimu kufanya vipimo mapema na kutibu mapema ugonjwa, kwa maneno mazuri ni kwamba kadiri unavochelewa kutibu magonjwa ya zinaa ndivyo unaongeza hatari zaidi ya kupata athari kubwa kwenye uzazi.


-Jikinge na maradhi ya bacteria na maambukizi mengine

Baadhi ya njia unazoweza kutumika kuzuia kutokea kwa maambukizi ni

Usitumie sabuni zenye kemikali- kuosha uke kwa kutumia sabuni zenye kemikali na kemikali hufanya tishu za uke kututumka, kuharibu uwiano wa bacteria kenye uke na pia kupunguza tindikali iliyopo mpaka kupelekea kuongezeka kwa uchafu unaotolewa

Ukiwa kwenye hedhi tumia pedi zisizo na kemikali, pedi za asili zisizo na harufu kali. Hii itasaidia kuzuia ukuaji wa bacteria kwenye uke.

Hakikisha unaimarisha kinga yako ya mwili : unapokuwa na kinga imara basi unajikinga dhidi ya kushambuliwa na magonjwa ya zinaa. Unaweza kutembelea stoo yetu kwa kubonyeza hapa ili upate virutubisho vya kuimarisha kinga yako.

-Epuka kujisafisha kwa kuingiza kidole hadi ndani. Kujisafisha hivi kunaharibu mpangilio wa kawaida wa bacteria kwenye uke(normal flora). Pia unapotumia kemikali na spray kujisafisha unaua bacteria wazuri na kuongeza athari na ahatari ya kupata maambukizi.


ANGALIZO NA TAHADHARI KWA WAGONJWA WA PID.


Endapo utagundua kwamba unapata dalili za magonjwa ya zinaa kama tulivoelekeza hapo juu mfano maumivu ya tumbo chini ya kitovu, maumivu wakati wa kujamiiana, maumivu wakati wa kukojoa, hedhi kuvurugika, mamumivu makali wakati wa hedhi, na mengine, basi hakikisha unamuona Daktari mapema kwa ajili ya vipimo.


WASILIANA NASI KWA USHAURI NA MSAADA JUU MAGONJWA SUGU PIGA 0688426300/0762291606


Post a Comment

0 Comments