Subscribe Us

header ads

JE? UNAFAHAMU KWA NINI UNAPATA MAUMIVU MAKALI YA MAUNGIO YA MIFUPA (JOINT)?

"JE . UNAFAHAMU KWA NINI UNAPATA MAUMIVU YA MAUNGIO YA MIFUPA(JOINTS)?

Leo tutazungumzia tatizo linalowapata watu wengi sana pale umri wao unapokuwa umezidi miaka 50 na hasa wale wenye miili mikubwa.

Nina uhakika kuwa umewaona akina mama wenye umri mkubwa na miili mikubwa wanavyopata shida kutembea huku wakiinama toka upande mmoja hadi mwingine kila wakipiga hatua au shida wanayopata pale inapowabidi kupanda ngazi au kukuchuchumaa. Maneno kama “ugonjwa wa kuumwa Mifupa, nina tatizo la joints, maumivu ya Mgongo” Au maumivu ya Kiuno Na Nyonga,Nadhani umeyasikia mara nyingi. Tatizo hasa hapa ni nini? Ungana nami katika mada hii uujue ugonjwa huu wa Mifupa kitaalamu(arthritis).

UGONJWA WA ARTHRITIS NI NINI?

Arthritis ni ugonjwa unaotokana na namna yo yote ya hitilafu katika maungio ya mifupa ya binadamu ambao husababisha maumivu Makali Sana na pengine kuvimba katika sehemu moja au zaidi ya maungio hayo. Neno arthritis halilengi ugonjwa mmoja bali jamii ya magonjwa ambayo kwa ujumla yapo zaidi ya 100. Tabia kuu ya magonjwa haya ni maumivu kwenye maungio ya mifupa (joints) ambayo ni endelevu na ambayo hutokea eneo hilo moja.

CHANZO CHA ARTHRITIS NI NINI?

Kusudi kuelewa chanzo cha ugonjwa huu, hebu kwanza tutazame muundo wa joint au sehemu mifupa miwili inapokutana. Fikiria goti ambapo mifupa miwili mmoja wa paja na mwingine wa mguu vinapokutana maungio ya mifupa.


LIGAMENTS: 

Ndicho kitu kinachoshikilia mifupa hii miwili pamoja. Hii ni kama utepe wa plastiki au mpira unaonyumbuka uliozunguka eneo hilo kwa nje, ukikunja goti inanyumbuka na ukinyoosha mguu inarudi.

CARTILAGE:

Huu ni utando unafunika eneo ambalo mifupa hugusana ili kuzuia mifupa hii isisuguane moja kwa moja. Utando huu ambao kwa kiswahili tunauita gegedu huyawezesha maungio hayo kufanya kazi kiulaini pasipo kusababisha maumivu.

CAPSULE:

 Hiki ni kitu kinachofunika maungio haya kikizunguka pande zote. Ndani ya mfuko huu wa capsule kuna synovial fluid ambayo huzalishwa na synovial membrane. Synovial fluid ni ute wa kulainisha sehemu hiyo ya maungio na synovial membrane ni utando ulio kwenye kuta za ndani za capsule.

Ugonjwa wa arthritis unasababishwa na hitilafu yo yote katika sehemu hizo za maungio ya mifupa. Inaweza kuwa cartilage inalika, upungufu wa Madini Kwenye Mifupa Au synovial fluid(Ute), maambukizi ya vijidudu katika moja ya maeneo hayo au mchanganyiko wa matatizo.

SABABU  NYINGINE ZINAZOPELEKEA MAUMIVU MAKALI YA MIFUPA NA MAUNGIO 

👉🏻kujichua muda mrefu hupelekea maumivu hayo.

👉🏻Namna ya kulala (style) /godoro Au Matumizi Mabaya Ya mto inaweza kukusababishia maumivu hayo

👉🏻Kufanya Kazi Nzito Kama Kubeba mizigo kwa kuinama 

👉🏻Uzito Mkubwa Au kunenepa wakati wa ujauzito

👉🏻Kukaa Au Kusimama Kwa Muda Mrefu Huathiri Mifupa na kupelekea Maumivu Makali.

 MADHARA YA MAUMIVU YA NYONGA NA KIUNO

👉🏻Hupelekea kushindwa kufanya tendo la ndoa

👉🏻Hupelekea kupooza kwa baadhi ya viungo vya mwili

👉🏻Hupelekea kuwahi kufika kileleni mapema wakati wa tendo na kushindwa kurudia

👉🏻Unaweza kushindwa kutembea kabisa /kunyanyuka, utakaa ukiwa umelala.

MATIBABU:-

Siku Zote Matibabu Bora Ni Yale Yanayolenga kushughulikia Chanzo Cha Tatizo Hivyo Ni Vyema Ukawasiliana Na Mtoa Huduma Za Afya Aweze Kupata Historia Ya Tatizo,Chanzo,Aina Ya Matibabu Uliyopitia Na Ukubwa Wa Tatizo Ili Kuweza Kutoa Suluhisho La Kudumu Litakalo Maliza kabisa Tatizo Lako.

 ANGALIZO 

👉🏻Kuna sababu nyingi zinazopelekea maumivu ya Maungio Ya Mifupa na baadhi ya sababu hizo huashiria magonjwa hatari ni Vyema Ukafahamu Kwanza Chanzo Cha tatizo Kabla ya Matibabu.

Je? Unasumbiliwa Na Maumivu Makali Ya Maungio  Ya Mifupa Na Misuli? Lipo Suluhisho Kwa Ajili Ya Tatizo Lako, Tupigie Simu Sasa Kwa Ushauri[BURE]

Piga Simu 0688426300 Au 0745885588


Facebook/instagram Afya Ya Mifupa Na Viungo Tanzania

Post a Comment

0 Comments