FAHAMU NJIA RAHISI YA KUONDOA CHUNUSI MWILINI KWA WANAWAKE NA WANAUME.
Emmanuel jiguwi
0688426300
Chunusi ni vipele vinavyojitokeza katika ngozi hususan sehemu za usoni, kifuani na mgongoni kutokana na mafuta kushindwa kutoka kwenda nje ya mwili (juu ya ngozi ya nje). Huweza kutokea kwa mtu yeyote aliyepevuka kimwili, japokuwa wanawake hutokewa zaidi na vipele hivi.
SABABU ZA ZINAZOPELEKEA KUWA NA CHUNUSI
Sababu kubwa ya chunusi ni kukaa kwa mafuta chini ya ngozi ya nje na kusababisha uvimbe. Hii inatokana na mafuta hayo kuzalishwa kwa wingi zaidi au kushindwa kupita kwenye matundu ya kutolea mafuta kwa sababu matundu hayo yameziba.
Pia bakteria wa chunusi huweza kushambulia ngozi na kusababisha chunusi au kuzifanya chunusi kuwa nyingi zaidi na kubwa kubwa
Vitu vinavyosababisha au kuongeza ukubwa wa chunusi ni pamoja na
1. Kiasi kikubwa cha mafuta kwenye ngozi
2. Kuziba kwa matundu ya kutolea mafuta kwenye ngozi
3. Homoni za uzazi mwilini (Androgens)
4. Msongo (Stress)
5. Maambukizi ya bakteria wanaosababisha chunusi
6. Kemikali (vipodozi) kali au zisizoendana na ngozi ya mtu
7. Aleji (Mzio) kwa baadhi ya vipodozi na kemikali zingine
8. Baadhi ya vyakula (vinavyotokana na maziwa, chipsi na chokoleti)
NINI CHA KUFANYA KAMA UNA CHUNUSI.
Ukitokwa na chunusi cha kwanza hakikisha unakuwa mwangalifu ili usiziongeze zaidi. Tafuta sababu insayozisababisha na kisha iepuke au iondoe hiyo kwanza
Cha pili epuka kupasua chunusi. Kupasua chunusi husababisha makovu chunusi zitakapopona
Tatu tafuta matibabu na uanze matibabu mapema. Ni rahisi zaidi kutibu chunusi ukiziwahi kuliko ukiwa umechelewa
MATIBABU YA CHUNUSI
Matibabu ya chunusi hutegemea na ngozi ya mtu na chanzo kinachosababisha hizo chunusi. Matibabu hayo mara nyingi hulenga kuua bakteria wanaosababisha chunusi hizo, kupunguza mafuta na kuzibua matundu ya kutolea mafuta ili mafuta yaweze kupita na kwenda nje ya ngozi.
1. Kuua Bakteria wanaosababisha Chunusi
Bakteria hawa huuliwa kwa kutumia dawa za kuua bakteria zijulikanazo kama Antibiotics. Utaalam na umakini unahitajika katika matumizi ya dawa hizi Pia ni lazima zitumike kwa maelekezo ya daktari
2. Kupunguza mafuta juu ya ngozi na kuondoa mafuta yaliyoziba matundu ya mafuta
Hii ni njia kubwa sana na rahisi ya kukabiliana na chunusi. Kwa kuwa mafuta ni sababu kuu kwa watu wengi basi njia hii husaidia watu wengi sana.
Hili huweza kufanywa kwa kutumia
- Sabuni za PROTEX (Iliyoandikwa DEEP CLEAN) na PEARS (Iliyoandikwa OIL CLEAR)
- Poda ya POND’S (Iliyoandikwa OIL CONTROL)
- Sabuni za maji za kusafishia uso na kuondoa uchafu na mafuta ya ziada (Face Wash au Facial Cleansers)
3. Kuondoa uchafu wote na seli zilizokufa na kuziba matundu ya kutokea mafuta kwenye ngozi
Njia hii hufanya kazi vizuri sana pia. Uchafu huo na seli zilizokufa zikiondolewa mafuta hupita vizuri na kwenda nje ya ngozi bila kusababisha chunusi. Matokeo yake mtu hupona chunusi na pia kuzizuia zisijitokeze.
Hili hufanywa kwa kutumia dawa zinazoondoa utando wa uchafu na seli zilizokufa zilizopo juu kabisa ya ngozi.
Mifano yah ii ni Persol Gel
MUHIMU:
- Ili kudhibiti vizuri chunusi na kuziondoa kabisa unahitajika kujua kwa usahihi kabisa chanzo cha chunusi hizo na vinavyoziongeza
- Mara nyingi chunusi hutibiwa kwa kutumia zaidi ya dawa moja au kipodozi kimoja. Jua vizuri mchanganyiko wa dawa na vipodozi vya kutumia
- Tumia dawa na vipodozi vinavyoendana na ngozi yako. Tofauti na hapo chunusi zitaongezeka zaidi
- Kutibu chunusi vizuri na kwa usalama kunahitaji muda. Kuwa mvumilivu na tumia vitu vyote kama ulivyoelekezwa
- Usipasue chunusi. Utabaki na makovu ambayo nayo pia yatakusumbua
Kwa maelezo zaidi, ushauri na matibabu ya Chunusi, Makovu, Madoa, Mafuta mengi usoni tafadhali wasiliana kwa kubofya link hii chini sasa hivi Au Piga 0688426300
https://wa.me/255688426300
SHARE MARA NYINGI UWEZAVYO MUNGU ATAKUBARIKI
0 Comments