JINSI YA KUONDOA MAKUNYANZI AU MIKUNJO KATIKA NGOZI HASA USONI(wrincles,aging)
Makunyanzi ni kitendo cha ngozi ya juu ya binadamu kupoteza umbo lake la wali na kuwa dhaifu hivyo kujikunjana kuchora mistari mistari hivyo kufanya ngozi kuwa dhaifu na kupoteza mvuto na uhalisia wake!
SABABU KUU YA MAKUNYANZI NI KUDHOOFIKA KWA COLLAGEN ZA NGOZI AMBAZO HUIFANYA NGOZI KUWA IMARA NA AFYA!
COLLAGEN NI NINI
Collagen ni protini ngumu, isiyoyeyuka na iliyoumbwa kama nyuzinyuzi. Protini hii inayotengenezwa na amino acids hufanya theluthi moja ya protini yote iliyomo ndani ya mwili. Kuna aina nyingi za collagen, kama aina 16 hivi. Collagen hizi za ndani ya mwili ni ngumu sana na aina nyingine za collagen ni ngumu kuliko hata chuma.
Collagen hupatikana zaid kwenye ngozi na mifupa na hufanya kazi ya kuupa mwili uimara na nguvu ikiambatana na elastin. Kwenye tabaka la dermis, collagen hasaidia kujenga mtandao wa nyuzinyuzi unaosaidia seli mpya kukua juu yake. Kwa vile uzalishaji wa collagen mwilini hupungua na umri, ngozi hupoteza hali yake ya kunyumbuka na kuifanya ngozi kubonyea chini. Hivyo, mistari na mikunyanzi hujitokeza. Kupungua kwa collagen husababisha pia
udhaifu wa cartilage kwenye maungio ya mifupa (joints). Collagen huzalishwa na seli mbalimbali lakini haswa na seli za kuunganisha viungo (connective tissue cells). Mwili wa binadamu huendelea kuzalisha collagen vizuri hadi umri wa mtu unapofikia miaka 40 hivi, baada ya hapo uzalishaji hupungua na kuwa kidogo sana umri unapofika miaka 60.
Collagen hutumika kuondoa mistari na mikunyanzi ya juu ya ngozi (kuondoa wrinkles) na pia husaidia kuondoa makovu juu ya ngozi, yale ambayo hayana ncha kali. Collagen inayotumika inatokana na binadamu na wanyama wa jamii ya ng’ombe.
Collagen ni protini ambayo, kama protini nyingine inatengenezwa na amino acids. Kuna amino acids 9 ambazo ni muhimu katika utengenezaji wa collagen na ambazo hupatikana kutokana na chakula tunachokula . Chakula kizuri kwa kutoa collagen ni kile kinachotokana na wanyama, kama vile; jibini, mayai, samaki, maziwa na nyama ya kuku.
VITU VINAVYOSABABISHA UDHAIFU WA COLLAGEN NA KULETA MAKUNYANZI
JUA
MATUMIZI YA VIPODOZI HASA VYENYE STEROIDS
UVUTAJI WA SIGARA
MSONGO WA MAWAZO
UKOSEFU WA VYAKULA VYENYE PROTEIN NA KABOHYDRATE
KUTOKUNYWA MAJI MENGI
MUDA MDOGO WA KULALA
HOMONI
UKOSEFU WA VYAKULA NA MBOGAMBOGA MWILINI
POMBE
NA MENGINEYO
MAMBO HAYO HUSABABISHA MAKUNYANZI HASA USONI KWA HARAKA ZAIDI:
VITU AMBAVYO HUTOA MAKUNYANZI KWA HARAKA SANA
KAROTI
MAZIWA MGANDO
PARACHICHI
TANGO
PAPAI
KIINI CHA YAI
ALMOND OIL
kuna njia rahisi sana ambazo zina uwezo wa kutatua tatizo la mikunjo bila kuhaha katika maduka ya vipodozi kutafuta losheni au vipodozi ili kukabiliana na tatizo hili. Sasa unaweza kutumia vitu vya kawaida kabisa kuondoa mikunjo kwa urahisi na kuufanya uso wako uonekane kijana zaidi. Baadhi ya njia hizi ni kama;
Kutumia tango,yai na limao
vijiko 2 vya juisi ya matango
ute mweupe wa yai
kijiko kimoja cha maji ya limao
Maandalizi:
changanya vitu hivyo kwenye chombo kimoja na hakikisha kwamba vitu vyote vimechanganyika sawasawa. Hifadhi mchanganyiko huo tayari kwa kuupaka kwenye uso.
TANGO
LIMAO
UTE MWEUPE WA YAI
Jinsi ya kutumia:
osha uso wako kwa maji na sabuni na hakikisha umeukausha baada ya kuosha uso wako
pakaa mchanganyiko wako ulioandaa kwenye uso wako na acha mchanganyiko huo bila kunawa kwa muda wa dkk 15 hadi 20 kabla ya kuosha uso wako
osha uso wako kwa kutumia maji ya uvuguvugu
JE?UNASUMBULIWA NA CHANGAMOTO YEYOTE YA AFYA PIGA 0688426300 AU 0762291606 KWA USHAURI BURE NA SULUHISHO KULINGANA NA CHANZO CHA TATIZO.
PIA UNAWEZA CHATI NA MIMI KUPITIA WHATSAPP YANGU KWA KUBOFYA LINK CHINI
https://wa.me/255688426300
0 Comments