Subscribe Us

header ads

Je? Unafahamu Nini Kuhusu Ngiri Ya Uti Wa Mgongo?


 Ngiri Ya  Uti Wa Mgongo Ni Nini? Umewahi Kusikia Hii?


 (Herniated Disc)


Aina hii ya ngiri hutokea pale pingili moja au zaidi, katika uti wa mgongo inapopata mushkeli unaopelekea gamba la nje la pingili husika kupata ufa. 


Kupitia ufa husika sehemu ya ndani ya pingili, ambayo kwa kawaida ni laini, hupenya nje.


Mara nyingi ngiri ya mgongo hutokea zaidi katika pingili za chini, karibu na kiunoni, au katika pingili za shingo.


Kwa kawaida aina ya maumivu ya mgonjwa yatategemea na aina ya pingili iliyoathirika. Maumivu ya mgongo karibu na kiunoni ambayo mara nyingi yanahusisha makalio, mapaja na hata miguu ni kiashiria cha kuathirika kwa pingili za sehemu ya chini ya mgongo.


Maumivu ya mgongoni, kwenye maungio ya shingo na mabega, ni kiashiria kuwa pingili iliyoathirika ni ya shingoni. 


Athari kwenye pingili hizi inaweza ikapelekea pia mhusika akapata maumivu ya mabega pamoja na mikono.


Ukiondoa maumivu ya kawaida, ngiri ya mgongo inaweza ikasababisha pia ganzi, na maumivu kama ya kuungua au kuchomwachomwa na sindano, iwapo ngiri hiyo itakuwa imeathiri mishipa ya fahamu inayowasiliana na hayo maeneo yenye ganzi au maumivu.


Iwapo wewe mwenyewe binafsi, au jamaa yako, mna tatizo la ngiri ya mgongo basi tafuta uwezekano wa kuwasiliana nasi Afya Ya Mifupa Na Viungo Tanzania


Tangu mwezi December 2017 Afya Ya Mifupa Na Viungo Tanzania Tumewasaidia  Zaidi Ya Watu 60 wenye Ugonjwa wa ngiri ya mgongo kwa mafanikio makubwa.


Wasiliana Nasi Sasa Kwa Suluhisho La

 Kudumu Piga 0688426300/0762291606


#Emmanueljiguwi #herniateddisc #spinacord

#Afyayamifupanaviungotanzania #Upasuaji

#Ngiriyautiwamgongo #sarataniyamufupa

#Maumivu #kiuno #nyonga #remathoid #Knee.

Post a Comment

0 Comments